Monday, November 11, 2013

Rekodi ya ufungaji yapanda Ligi Kuu

Kikosi cha Simba Na Abducado Emmanuel, Dar es SalaamCHATI ya ufungaji mabao katika Ligi Kuu ya Vodacom, imeonekana kupanda kwa kasi msimu huu kutokana na mabao 207 kufungwa hadi kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo tofauti na msimu uliopita.Msimu uliopita baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza, jumla ya mabao 196 yalifungwa lakini msimu huu kuna tofauti kubwa kutokana na idadi ya mabao yaliyofungwa.Timu za Simba, Mtibwa Sugar na...

Tanzanite yatua Dar kuivutia kasi Afrika Kusini

Timu ya Taifa Wanawake walio chini ya umri wa miaka 20 (Tanzanite) Na John Dande, Dar es Salaam:      TIMU ya Taifa ya Wanawake walio chini ya umri wa miaka 20 (Tanzanite), imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1, baada ya juzi kuinyuka Msumbiji mabao 5-1.Mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo, yalifungwa na...

Uchaguzi Mkuu TBF Desemba 10

Na Mohamed Mharizo, Dar es Salaam:UCHAGUZI mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), unatarajia kufanyika Desemba 10 mwaka huu jijini Mbeya.Kwa mujibu wa Rais wa TBF, Mussa Mziya, uchaguzi huo unafanyika kwa mujibu wa katiba baada ya uongozi uliopo madarakani kumaliza muda wake. “Napenda kuchukua fursa hii kutoa tangazo rasmi la tukio la uchaguzi mkuu wa viongozi wa TBF utakaofanyika Desemba 10 mwaka huu jijini Mbeya na kikatiba inabidi ufanyike uchaguzi kuwapata viongozi wapya watakaoendesha shughuli za shirikisho kwa miaka minne ijayo,”...